VATICAN CITY, Vatican
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Leo XIV amekutana na kuzungumza na kikundi cha wanahija kutoka Parokia ya Mtakatifu Thomás wa Villanuova - Alcalá ya Henares nchini Hispania.
Katika hotuba yake kwa lugha ya kihispania, Papa alionesha furaha yake kukutana nao katika siku ya Oktava ya Noeli na kuwakaribisha sambamba na kuzungumza nao mambo mbalimbali.
Kama Jumuiya ya Parokia, alisema kwamba waliweza kujiandaa kwa jitihada kubwa katika hija ya kijubilei na wakati wa mwaka huu kwa namna ya pekee kwa Kanisa ambapo walimsindikiza Mfuasi wa Mtume Petro kwa sala zao na kwa ukarimu wao.