DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wamesema wamekumbwa na mashaka kuhusu matumizi ya michango yao.
Kwa nyakati tofauti, wanachama hao wamesema hawana imani kama michango yao bado ipo salama kutokana na hali ya namna ilivyokuwa ikiendeshwa ndani ya CWT.