Dar es Salaam
Na Nicolaus Kilowoko
Uongozi wa Klabu ya Soka ya Singida Black Stars kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano, Hussein Massanza umeendelea kukazia kuwa wachezaji wanaocheza ndani ya klabu hiyo hawatoondoka, licha ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kutimkia katika timu kubwa za Simba, Yanga na Azam FC.
Massanza alisema kuwa wao wanawashanga wapinzani wao na kuwacheka, kwani kila kukicha wachezaji wao wanahusishwa kwenda kwao lakini bado wanakipiga ndani ya timu ya Singida.