Na Nicolaus Kilowoko
Kocha wa zamani wa Yanga Princess, Edna Lema ‘Mourinho’, ambaye kwa sasa ameongezwa kwenye Benchi la Ufundi la kikosi cha Wanaume cha Yanga, amekiri kuvutiwa na uwezo wa mchezaji Pacome Zouzoua.
Edna ambaye ameunganishwa katika kikosi cha wanaume mara baada ya Ligi ya wanawake kusimama, hivi karibuni ameonja ushindi wa kwanza mara baada ya timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.
Alisema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao anavutiwa nao na wenye uwezo, uzoefu, akili na maarifa wakiwa uwanjani ni Pacome ambaye kwa sasa ana mabao nane kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu.