Print this page

Brazil kushusha rungu kwa wanaosimama juu ya mpira

Memphis Depay Memphis Depay

LONDON, ENGLAND
Mshambuliaji wa Corinthians Memphis Depay amekosoa uamuzi wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF), kuwaadhibu wachezaji kwa mbwembwe za kusimama juu ya mpira wakati wa mechi.
CBF imetangaza kwamba wachezaji wanapaswa kuonyeshwa kadi ya njano, iwapo watasimama juu ya mpira kwa miguu yote miwili, na timu pinzani ikapewa mkwaju wa faulo usio wa moja kwa moja.
Uamuzi huo ulikuja baada ya Depay kufanya hatua hiyo katika dakika za majeruhi, wakati wa ushindi wa fainali ya Paulista A1 dhidi ya Palmeiras mnamo Machi 28.
Ustadi huo, uliochezwa karibu na bendera ya kona baada ya Depay kujifanya kuvuka mpira ndani ya kisanduku, uliwakera wachezaji wa Palmeiras na kuzua rabsha kubwa kati ya timu zote mbili.
Kipa wa akiba wa Palmeiras, Marcelo Lomba na kiungo wa kati wa Corinthians, Jose Martinez walitolewa nje baada ya ukaguzi wa muda mrefu wa VAR, ambao ulisababisha zaidi ya dakika 18 za muda wa nyongeza, kuongezwa na maafisa.
Katika barua iliyofuata kwa vilabu, CBF ilisema kwamba kitendo cha kusimama kwenye mpira ni chokozi kwa mpinzani na kutoheshimu mchezo.

Rate this item
(0 votes)
Japhet