Print this page

Mourinho amlilia Baba Mtakatifu

ANKARA, Uturuki
Kocha Jose Mourinho ametoa heshima za dhati za kuguswa na kifo cha Baba Mtakatifu Fransisko, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 88.
Mourinho, ambaye kwa sasa anainoa Fenerbahce lakini hapo kabla amewahi kuzinoa Chelsea, Tottenham na Manchester United za Uingereza, alitumia ukurasa wa Instagram kumuenzi Baba Mtakatifu  Fransisko.
Mreno huyo aliandika: “Ili kuwa mkuu, zaidi ya yote unahitaji kujua jinsi ya kuwa mdogo. Unyenyekevu ni msingi wa ukuu wa kweli. Papa Fransisko. Matumaini ni mwanga usiku. Grande Papa.”
Baba Mtakatifu ambaye aliugua ugonjwa wa mapafu na sehemu ya pafu moja kuondolewa akiwa kijana, alilazwa katika hospitali ya Gemelli mnamo Februari 14 kwa shida ya kupumua ambayo ilikua ni nimonia.
Alitumia siku 38 huko, muda mrefu zaidi wa kukaa hospitalini kwa upapa wake wa miaka 12.
Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Italia, Serie A vilituma salamu za heshima kwa Papa, kufuatia kifo chake ikiwemo timu kongwe ya AS Roma.
“Roma inaungana na kuomboleza kifo cha Papa, msiba ambao unahuzunisha sana jiji letu na ulimwengu mzima,” Roma ilisema katika taarifa.

Rate this item
(0 votes)
Japhet