Dar es Salaam
Na Mwandishi wetu
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia-Goba Mwisho, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Musa Kihoo, amewataka Waamini kufuata mafundisho ya Bwana Yesu Kristo, kwa sababu yeye ni njia ya ukweli ya kwenda Mbinguni.
Padri Kihoo alisema hayo wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu, Kuabudu Msalaba Mtakatifu iliyofanyika parokiani hapo.
Padri Kihoo alisema kwamba Waamini wengi wanamchukiza Bwana Yesu Kristo kwa kutenda dhambi, ikiwemo kusema uwongo, umbeya, kusengenya wenzao, kunyanyasa wapangaji na ujambazi.