Print this page

Watoto wajengwe kiimani - Askofu

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akizungumza na vijana wa Kipaimara kabla ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mungu - Vijibweni, jimboni humo. (Picha na Mathayo Kijazi) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akizungumza na vijana wa Kipaimara kabla ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mungu - Vijibweni, jimboni humo. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Wazazi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Maparoko katika parokia zao, ili watoto wao waendelee na mafundisho ya kuwajengwa katika imani baada ya sakramenti zao.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mungu - Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Wazazi na walezi toeni ushirikiano kwa Paroko wenu, ili watoto hawa waendelee kupatiwa majiundo, waendelee kupatiwa Mafundisho ya Imani hata baada ya kupokea Sakramenti hii ya Kipaimara,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aidha, Askofu huyo aliwataka vijana kuwa watumishi wa Bwana kikamilifu, huku wakiitambua hadhi yao pamoja na wito wao.
Alisiwahi kuwa watumishi kweli wa Yesu Kristo, badala ya kuwa Wakristo goi goi, wala Wakristo tia maji tia maji katika maisha yao
“Kuweni watumishi kweli wa Yesu Kristo, msiwe Wakristo goi goi, wala Wakristo tia maji tia maji katika maisha yenu. Itambueni hadhi yenu na wito wenu kama Wakristo,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aliongeza kuwa kwa kupokea Sakramenti hiyo Takatifu ya Kipaimara, sasa vijana hao wamehitimisha awamu ya kuwa watoto, akiwasihi kudumu katika imani, huku wakiyashika yale yote waliyofundishwa.
Aliwasihi kuendelea kuimarisha imani na maadili, akimsihi Paroko wa parokia hiyo kusimamia ili vijana hao waendelee kupatiwa mafundisho (majiundo), endelevu.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema kwamba kwa kuwa hizi ni zama za kelele, upo umuhimu wa kuwasimamia vyema watoto hao ili waendelee kukua katika misingi ya imani, kwani wasiposimamiwa vyema, watapotea.
Katika homilia yake, Askofu huyo aliwasihi vijana, wazazi na Waamini wote kwa ujumla, kupendana kama vile Kristo anavyowapenda, kwani Kristo amewapenda bila kujibakiza.

Rate this item
(0 votes)
Japhet