Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama Mhashamu Christopher Nkoronko, (pichani) amewataka Waimarishwa kuwa tofauti na wengine hasa wanapokuwa kanisani, nyumbani au shuleni.
Alisema hayo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, iliyofanyika katika Parokia ya Watakatifu Joachim na Anna-Mwime Jimbo Katoliki la Kahama.