Dar es Salaam
Na Laura Mwakalunde
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amewasihi Waamini kuacha kuzificha imani zao kwa kubadilika badilika kila wakati.
Aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Martha- Mikocheni jimboni humo.