NAIROBI, Kenya
Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaraza ya Maaskofu Wanachama Afrika Mashariki (AMECEA), Padri Anthony Makunde wakati wa uzinduzi wa Sera ya Mawasiliano ya AMECEA, ameeleza kuwa waraka huo unaweza kutumika kama mwongozo wa mikutano mingine katika kanda hiyo, wakati wa kuandaa sera zao za mawasiliano.
Akiwahutubia washiriki mtandaoni na waliokuwepo wakati wa uzinduzi, katika Madhabahu ya Consolata jijini Nairobi, Kenya, Padri Makunde alisema “Sera ya Mawasiliano ya Kijamii sio waraka wa ndani wa Sekretarieti tu, bali inakusudiwa kutumika kama marejeleo ya mikutano ya wanachama na dayosisi, wakati wanaunda sera zao za mawasiliano kitaifa na Jimbo.