Print this page

Papa kuzuru kituo cha Laudato si

Kituo cha Borgo Laudato kilichopo Castel Gandolfo kinachotarajiwa kuzinduliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV. Kituo cha Borgo Laudato kilichopo Castel Gandolfo kinachotarajiwa kuzinduliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV.

VATICANCITY, Vatican

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Leo XIV, anatarajia kutembelea na kuzindua sehemu iliyoanzishwa kwa matakwa ya hayati Papa Fransisko, sanjari na kuadhimisha Liturujia ya Neno na Baraka ya kituo cha Borgo Laudato si.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mawasiliano ya Kituo cha Mafunzo ya Juu ya Laudato si, inaeleza kwamba ziara hiyo itafanyika Septemba 5 mwaka huu, na kwamba tukio hilo linatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni masaa ya Ulaya, ili kuzindua rasmi Borgo Laudato si, mahali ambapo kwa karne nyingi yamekuwa ni makazi ya Mapapa, ambayo sasa yamefunguliwa kwa umma, na ambapo kanuni zilizomo katika Waraka wa Kitume wa Laudato si’, mwaka huu zinaadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake.

Rate this item
(0 votes)
Japhet