Dar es Salaam
Na Mathayo Kijazi
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, ametoa ufafanuzi na kukanusha kwamba si kweli kwamba Wakatoliki wanaabudu sanamu, bali wanamwabudu Bwana Yesu Kristo, aliyejinyenyekesha, akatii mpaka kufa msalabani.
Aliyasema hayo hivi karibuni, katika homilia yake wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu, ya Sikukuu ya Fumbo la Kutukuka kwa Msalaba, iliyofanyika katika kituo cha Hija – Pugu, jimboni humo.