Mbozi
Na Mwandishi Wetu
Katika hatua muhimu ya kupunguza upofu, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) na Shirika la Helen Keller International, leo wamewasili mkoani Songwe kwa ajili ya kutoa Huduma Mkoba ya matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho “Cataract Management”, kwa wananchi takribani 700 wa Songwe, katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi (Vwawa).
Akiongea na Waandishi wa Habari, Dk. Jofrey Josephat Mratibu wa Huduma za macho Mkoa wa Songwe, alieleza kuwa kambi hiyo ya siku sita imelenga kukabiliana na magonjwa ya mtoto wa jicho, na kusogeza huduma hizo adimu katika maeneo ya karibu na wanapoishi (vijijini), ambapo imekuwa ngumu kupatikana na gharama kwa wananchi, kuzifuata katika hospitali kubwa.