Bukoba
Na Mwandishi wetu
Balozi na Mwanadiplomasia wa Vatican, Mhashamu Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ambaye ni Mtanzania, amefariki Dunia Jumanne ya Septemba 16, mwaka huu mjini Roma nchini Italia.
Taarifa iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Jovitus Mwijage kwa Maaskofu, Mapadri, Watawa na Waamini ilieleza kwamba Askofu Mkuu Rugambwa aliaga Dunia wakati akipatiwa matibabu kutokana na changamoto za kiafya.