Dar es Salaam
Na Mathayo Kijazi
Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Cornelius Mashare, amewataka wazazi kutowalea watoto wao kama mayai, kwa kutowaruhusu wafanye kazi za nyumbani, kwani kufanya hivyo ni kutengeneza kizazi legelege.
Akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya shukrani kwa Mungu, kwa Mahafali ya 20 ya Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Kristo Mfalme, iliyoadhimishwa parokiani hapo, Padri Mashare alisema kwamba inasikitisha kuona kijana wa darasa la saba, hawezi kutandika hata kitanda, kuosha vyombo, wala kufanya kazi yoyote, ambayo vijana wengine wa umri wake wanaweza kufanya.