VATICAN CITY, Vatican
Hivi karibuni Padri Petro Paolo Oros, Mfiadini wa utawala wa Kikomunisti, aliyeuawa mwaka 1953 akiwa na umri wa miaka 36, ametangazwa kuwa Mwenyeheri.
Katika kutangazwa Mwenyeheri Padre huyo huko Bilky nchini Ukraine, Mwadhama Grzegorz Kardinali Ryś, Askofu Mkuu wa Łódź, nchini Poland, na Mwakilishi wa Papa, alisema kwamba katika dunia ya leo iliyosambaratishwa na vita vya kutisha, vilivyogawanyika zaidi ya hapo awali, na ambapo ubinadamu umepoteza uwezo wa kukutana kwa kina na unakabiliwa na upweke wa kutisha, Kanisa linahitaji watu wa kukutana na ushirika wa kweli, kama alivyokuwa Petro Paolo Oros.