VATICAN CITY, Vatican
na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher amesisitiza ukweli wa dharura wa hatari zinazozunguka maendeleo ya Akili Unde katika uwanja wa kijeshi, na kusema kuwa Teknolojia haipaswi kuchukua nafasi ya hukumu ya binadamu katika masuala ya maisha na kifo.
Askofu Mkuu Gallagher alisema hayo katika mjadala wa wazi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huko New York, nchini Marekani, ambapo alisisitiza kuwa wito wa Vatican ni kusitishwa mara moja kwa silaha hatari zinazojiendesha, na kusema kwamba ni hatari kutumia AI katika mifumo ya amri na udhibiti wa nyuklia.