Mwanza
Na Paul Mabuga
Katika harakati za kutafuta maisha kwa vijana kumekuwa na changamoto nyingi, wanazopitia, kwenye michakato yao ya kusaka maisha bora.
Miongoni mwa vijana ambao wamesaka maisha ni Anna Nicodemus, mmoja wa Wahariri katika kituo cha runinga, cha Shirika la Utangazaji la Namibia [NBC].
Yeye na timu yake walipanga kufanya filamu halisi [factual film], kama sehemu ya mafunzo ya chuo kimoja katika Jiji la Berlin, nchini Ujerumani. Na wameamua kuifanya kazi hii katika nchi yao.