Morogoro
Na Dk. Felician B. Kilahama
Mwenyezi Mungu aliumba kwa umakini mkubwa sana vyote viijazavyo dunia, ikiwemo misitu na mimea ya aina mbalimbali, na akauweka ulimwengu katika misingi imara isiyotikisika. Imeandikwa katika Biblia Takatifu Kitabu cha Mwanzo, Neno lake Mwenyezi Mungu linaeleza bayana kwamba:
“Mungu akasema nchi na itoe majani/nyasi, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambayo mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi, ikawa hivyo” (Mwanzo 1:11).
Aidha, vyote tunavyovishuhudia kuwepo katika ulimwengu, Mungu alivikamilisha ndani ya siku sita, na siku ya saba akapumzika baada ya kuona kila kitu kimekaa sawa.
Lakini Mwenyezi Mungu, alihitimisha yote kwa kumuumba binadamu kwa sura na mfano wake, mwanaume na mwanamke aliwaumba.