Print this page

Jubilei Miaka 25 Parokia ya Mbezi Louis yafana

Watoto wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu Parokia ya Mtakatifu Peter Claver – Mbezi Louis, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiimba wimbo maalumu wa Jubilei ya Miaka 25 ya Parokia hiyo. Watoto wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu Parokia ya Mtakatifu Peter Claver – Mbezi Louis, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiimba wimbo maalumu wa Jubilei ya Miaka 25 ya Parokia hiyo.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Parokia ya Mtakatifu Peter Claver – Mbezi Louis, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, imeadhimisha Jubilei ya Miaka 25, huku Waamini wakiaswa kuepuka dhuluma, kutafuta ukubwa, umaarufu na kutambulika katika jamii.
Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei hiyo, alisema kwamba:
“Hayo ni mahangaiko makubwa ya wanadamu, kupambana kupata ukuu, kupambana kupata umaarufu, kupambana kuwapiku wengine. Na katika kupambana huko, tunaweza tukatendeana visivyo, tukadhulumiana, tukakanyagana, tunaweza tukakuta mtu anatembea juu ya mabega na vichwa vya wengine ili aonekane, atambulike, aheshimike. Ukuu wa kweli hauji kwa kuwapiku wengine, ukuu wa kweli hauji kwa kuwakanyaga wengine,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Rate this item
(0 votes)
Japhet