Print this page

Waadhimisha Jubilei ya Mtakatifu Justin

By November 07, 2025 38 0
Askofu Mkuu Menghisteab Tesfamariam. Askofu Mkuu Menghisteab Tesfamariam.

ASMARA, Eritrea

Kanisa nchini Ethiopia na Eritrea, limeadhimisha Jubilei ya Miaka 50, ya kuinuliwa hadi utakatifu wa Mtakatifu Justin De Jacobis, kwa Misa Takatifu ya Shukrani iliyoongozwa na Askofu Mkuu Menghisteab Tesfamariam, akiambatana na wakubwa wa kidini na Mapadri zaidi ya 20, wa sherehe katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Msaada wa Daima-Kidane Mehret.
Katika barua yake kwa Waamini wote na makutaniko ya kidini nchini, Askofu Mkuu Tesfamariam, aliwaalika kushiriki katika tukio hilo maalumu la kumshukuru Mungu na kumheshimu Mtume wa Imani Katoliki nchini, Mtakatifu Justin de Jacobis, ambaye alipandishwa cheo na Baba Mtakatifu Paulo VI, mnamo Oktoba 26, 1975.

Rate this item
(0 votes)
Japhet