DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Waamini wametakiwa kufuata mafundisho ya Bwana Yesu Kristo na mwenendo wake, kwa kuwarithisha watoto wao Imani Katoliki.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni, na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Augustino-Salasala, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Peter Assenga, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekatisti.
“Mkristo kamili lazima awe amebatizwa na mwenye kushiriki Ekaristi Takatifu, na kufanya maungamo mara kwa mara,” alisema Padri Assenga.
Aidha, aliwasihi Waamini kutopokea Ekaristi Takatifu kama pipi, kwa sababu ni kufuru na ni dhambi.