Dar es Salaam
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kwamba huduma ya mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) katika barabara ya Morogoro kuelekea Kimara, Moroco na Barabara ya Kilwa kutoka katikati ya mji kwenda Mbagala imesitishwa kwa muda.
Hatua hiyo imetokana na kuaharibika kwa miundombinu ya barabara hizo.
Chalamaila (pichani) alitoa tamko hilo jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa Habari na kutaja kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua ya kufanya tathmini ya hasara iliyopatikana na kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo, hivyo pindi itakapokaa sawa huduma hiyo itarejea.
“Tumelazimika kusitisha huduma ya usafiri huo kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa uchaguzi na kundi la waandamanaji na kusababisha kuharibika kwa mifumo yote ya ukatajai tiketi na sehemu za kupakilia abiria hivyo sasa tunatoa maelekezo kwa LATRA kutoa vibali vya muda kwa wamiliki wa daladala hili waweze kuwahudumia wakazi wa maeneo hayo ambao kwa sasa wanahitaji kufika mjini,”alisema Chalamila.