Print this page

‘Sheria isiyomsaidia mtu haina maana’

By November 07, 2025 63 0
Mhashamu Askofu Lazarus Msimbe- SDS, wa Jimbo Katoliki Morogoro. Mhashamu Askofu Lazarus Msimbe- SDS, wa Jimbo Katoliki Morogoro.

Morogoro

Na Angela Kibwana

Mhashamu Askofu Lazarus Msimbe- SDS, wa Jimbo Katoliki Morogoro, amesema kuwa sheria ni kwa ajili ya watu na sio watu kwa ajili ya sheria, kwa sababu watu ni muhimu zaidi kuliko taratibu na sheria, kwani sheria isiyomsaidia mtu haina maana.
Askofu Msimbe alisema hayo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu, katika mahafali ya  wahitimu wa 14 wa Chuo cha Katekesi, ambapo kati yao wahitimu tisa ni kutoka Chuo cha Mtakatifu Karoli Lwanga-Mzumbe, na  watano kutoka Chuo cha Katekesi  cha Mtakatifu Yoseph Mfanyakazi Bigwa, iliyofanyika katika Chuo cha Katekesi Mzumbe jimboni Morogoro.
Askofu Msimbe kadiri ya tafakari ya Injili husika, alieleza kuwa huduma kwa watu ndio hitaji namba moja, kwa sababu dai la kwanza kwa yeyote ni dai la mahitaji ya binadamu, kwa kuwa sheria ambayo haimsaidii mtu haina maana.

Rate this item
(0 votes)
Japhet