Print this page

Wasafiri kujengewa Groto, kukinga ajali

By November 07, 2025 66 0
Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogath Kimario, akichimba msingi kuzindua ujenzi wa Groto ya Bikira Maria Mwombezi wa Wasafiri, kando ya Barabara ya Moshi-Arusha katika eneo la Maligo jimboni humo, wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi huo. Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogath Kimario, akichimba msingi kuzindua ujenzi wa Groto ya Bikira Maria Mwombezi wa Wasafiri, kando ya Barabara ya Moshi-Arusha katika eneo la Maligo jimboni humo, wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi huo.

Same

Na Mathayo Kijazi

Kutokana na kuwepo kwa matukio ya ajali za barabarani za mara kwa mara, Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogath Kimario, ameandaa mkakati wa kujenga Groto ya Bikira Maria Mwombezi wa Wasafiri, kando ya barabara katika eneo la Maligo jimboni humo, ili kusaidia kuzuia ajali hizo.
Askofu Kimario aliyasema hayo hivi karibuni, ambapo alibainisha kuwa eneo hilo mara nyingi hutumiwa na wasafiri, kama sehemu ya huduma za maliwato, hivyo ni vema kujenga Groto hiyo ili wasafiri wapate huduma za kiroho, ikiwemo kuombea safari zao.
Aliongeza kuwa wanafanya hivyo ikiwa pia ni sehemu ya maandalizi, kuelekea katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50, tangu Same ilipotangazwa kuwa Jimbo Katoliki, ambayo kilele chake ni Februari 3, 2027, hivyo katika kamati yao ya maandalizi, wameona ni vema kujenga Groto hiyo ya Bikira Maria Mwombezi wa Wasafiri.

Rate this item
(0 votes)
Japhet