Dar es Salaam
Na Laura Mwakalunde
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amewaonya Waamini kutoruhusu wao kuwa karakana ya shetani.
Alisema hayo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya uzinduzi wa nyumba ya Mapadri, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Consolatha-Mbezi Makabe.
“Kila Mkristo inampasa kuwa na maamuzi kwa kuachana na mambo ya kale, aibu ya giza, kwani inasikitisha kuona Mkristo anakwambia bado kidogo,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aidha, aliwataka Waamini watambue kuwa wao ni warumi wa leo, kwa sababu Mtume Paulo huwa anafundisha ukweli wa mambo ya kale, ya aibu na ya giza, kwa kutoruhusu akili na utashi wao kuwa kichaka cha dhambi.