Dar Es Salaam
Na Mwandishi Wetu
Katika kuadhimisha Wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imezindua rasmi kitengo kipya cha kusafisha damu (dialysis unit), kwa wagonjwa wa moyo wanaopata matatizo ya figo, hatua inayolenga kuboresha huduma za tiba jumuishi kwa wagonjwa hao.
Kitengo hicho chenye mashine za kisasa, zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200, kimeanza kutoa huduma mara moja baada ya kuzinduliwa, kikiwa na uwezo wa kusafisha damu kwa zaidi ya wagonjwa nane kwa siku.