Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu
Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), kinalaani vurugu, mauaji na uharibifu wa mali, vilivyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Chama hicho pia kimetoa pole kwa wote waliopoteza ndugu au mali, na kuunga mkono agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, la kufanya uchunguzi wa kina, na kuwawajibisha wahusika wote kwa mujibu wa sheria.