DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Mhifadhi Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa (NMT), Sechelela Magoile, amesema kuwa matumizi ya teknolojia yanapaswa kuiakisi jamii, na kuwawezesha Wananchi kupata taarifa sahihi, kuhusu maendeleo ya kisayansi, kukuza uelewa na kuweka jamii salama.
Alisema hayo katika kuadhimisha Siku ya Sayansi Duniani, iliyofanyika katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.