Print this page

COSTECH yahimiza ubunifu shuleni

By November 14, 2025 42 0

Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imewatembelea wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbwenitete jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Sayansi Duniani, kwa lengo la kuwahamasisha vijana hao kujikita katika ubunifu na matumizi ya sayansi, katika kutatua changamoto za kijamii.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu Mkuu wa Tafiti na Bunifu kutoka COSTECH, Dkt. Prosper Masawe, amesema kuwa amevutiwa na ubunifu mbalimbali uliooneshwa na wanafunzi wa shule hiyo, ambao unaonesha uwezo mkubwa wa kubuni suluhu za changamoto katika jamii.

Rate this item
(0 votes)
Japhet