LILONGWE, Malawi
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Lilongwe, nchini Malawi, Mhashamu Vincent Frederick Mwakhwawa, amewataka Waamini kudumisha heshima na uvumilivu wakati wa Misa, akisisitiza kwamba sherehe ya Ekaristi haipaswi kukatizwa kamwe, hata wakati wa changamoto.
Wito huo aliutoa hivi karibuni wakati wa ziara yake ya Kitume, katika Parokia ya Mtakatifu Paulo - Namitete, jimboni humo, ambapo yeye binafsi aliwashukuru na kuwatia moyo washiriki wa Utoto Mtakatifu (Watoto wa Wamisionari).