Morogoro
Na Angela Kibwana
Mhashamu Askofu Lazarus Vitalis Msimbe -SDS, wa Jimbo Katoliki Morogoro, ameongoza Misa Takatifu ya Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, Msimamizi wa Jimbo hilo, na kuwataka Waamini jimboni humo kukimbilia maombezi yake mara kwa mara, ili Jimbo liweze kustawi kiroho na kimaendeleo.
Adhimisho hilo lilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patris, jimboni Morogoro, iliyokwenda sambamba na kufunga mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya matumaini miaka 2025, jozi 44 za ndoa Takatifu, pamoja na kutoa shukrani kwa Mungu, kwa mavuno ya Tegemeza Jimbo mwaka huu 2025.