Dar es Salaam
Na Laura Mwakalunde
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amewataka Waamini kutambua kwamba, Karamu ya Sakramenti Takatifu haikuja ili kushibisha tumbo.
Askofu Ruwa’ichi alisema hayo hivi karibuni, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kuzindua Mnara wa Kanisa, iliyofanyika Parokia ya Mwenyeheri Anuarite-Makuburi, jimboni humo.