Mgeta
Na Angela Kibwana
Zaidi ya watoto Wamisionari 300 wa Shirika la Kipapa, Dekania ya Mgeta Jimboni Morogoro, wameshiriki Kongamano la kufunga mwaka, katika dekania hiyo.
Kongamano hilo limefanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli-Mgeta, Morogoro, likihusisha watoto kutoka Parokia sita zinazounda Dekania hiyo, kama njia mojawapo ya kuwakuza watoto kiimani na kimaadili, kupitia mafundisho ya semina na michezo mbalimbali.