Print this page

Uwanja wa Kriketi Melbone wakosa vigezo

Melboune, Australian
Uwanja wa Kriketi wa huko mjini Melbourne umekadiriwa kuwa hauridhishi, Baraza la Kriketi la Kimataifa (ICC) limethibitisha.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa, Uwanja wa Kriketi wa Melbourne unapata pointi moja ya upungufu. Ikiwa uwanja unapata pointi sita za upungufu katika kipindi cha miaka mitano, unasimamishwa kuandaa kriketi ya kimataifa kwa miezi 12.
Ni mara ya kwanza uwanja nchini Australia, kuonekana kuwa chini ya kiwango, tangu ICC ibadilishe mfumo wake miaka miwili iliyopita.
Wiketi thelathini na sita zilianguka katika vipindi sita katika mechi ya Boxing Day, huku harakati nyingi za kushona zikitolewa kwa wapiga mpira wa kasi.
“Kwa wiketi 20 zikianguka siku ya kwanza, 16 siku ya pili na hakuna mpigaji hata mmoja aliyefikia nusu karne, uwanja ulikuwa hauridhishi kulingana na miongozo, na uwanja unapata pointi moja ya upungufu,” alisema mwamuzi wa mechi Jeff Crowe.

Rate this item
(0 votes)
Japhet