London, Uingereza
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta, amekiri kuwa watakuwa wakiangalia kwa makini usajili unaowezekana, wakati wa dirisha la uhamisho la Januari.
The Gunners walitumia takribani pauni milioni 250 msimu huu wa joto, na kuleta wachezaji wapya nane, huku wakitafuta kuongeza ubora katika kikosi chao, ili kukabiliana na orodha ya mechi zilizojaa, na kushindania mataji katika mashindano mengi.
Msimu uliopita kampeni ya Arsenal iliharibiwa na majeraha, kwani walikuwa bila mlinzi Gabriel Magalhaes, kwa sehemu ya mwisho ya msimu na walicheza na kiungo Mikel Merino, kama mshambuliaji wa muda, walipomaliza wa pili katika Ligi Kuu kwa msimu wa tatu mfululizo, na walitolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa na Paris St-Germain.
Msimu huu The Gunners pia wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha, mara baada ya kumpoteza Kai Havertz tangu siku ya ufunguzi, huku nahodha Martin Odegaard na Bukayo Saka, Gabriel Martinelli, Noni Madueke na Max Dowman wakiwa wamekosa nafasi.
Sasa baada ya majeraha kuwaathiri zaidi wachezaji washambuliaji, ni safu ya nyuma ya Arsenal inayoteseka, Arteta alilazimika kumchezesha Declan Rice, katika nafasi isiyojulikana ya beki wa kulia dhidi ya Brighton siku ya Jumamosi, kwa sababu Jurrien Timber alikuwa majeruhi, na Riccardo Calafiori alipata tatizo wakati wa mazoezi ya kupasha misuli.