DAR ES SALAAM
Na Nicholas Kilowoko
Siku chache mara baada ya pambano lililomalizika, kwa Hassan Mwakinyo kumtandika bondia Stanley Eribo kutoka nchini Nigeria kwa ‘KO’, katika raundi ya pili ya pambano la raundi 10, bondia Twaha Kiduku ameubeza ushindi wake.
Bondia Twaha alisema kuwa pambano hilo lililofanyika siku ya Boxing Day, lilikuwa halina hadhi kutokana na mpinzani wa bondia mwenzake Mwakinyo, kutokuwa katika kiwango kinachotakiwa.