Print this page

Digitali yaweka ‘rehani’ maisha ya vijana nchini

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (kulia) Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba (wa pili kushoto) wakiwa katika maandamano kuingia katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Ufukweni Maarufu Beach Mass kwa ajili ya Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) iliyofanyika Jimbo Katoliki la Bagamoyo. (Picha na Laura Mwakalunde) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (kulia) Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba (wa pili kushoto) wakiwa katika maandamano kuingia katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Ufukweni Maarufu Beach Mass kwa ajili ya Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) iliyofanyika Jimbo Katoliki la Bagamoyo. (Picha na Laura Mwakalunde)

Bagamoyo

Na Laura Mwakalunde

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amesema kwamba  vijana wasipotumia vyema mifumo ya mitandao (digitali), itawaharibia maisha yao.
Askofu Mchamungu alitoa wito huo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya ufukweni (Beach Mass), iliyofanyika kwenye ufukwe wa Bahari, Jimbo Katoliki la Bagamoyo.
“Mambo yanayowakabili watu wengi na kuwaharibu Wakatoliki ni digitali, ambayo inaweza kuwavuruga na kusababisha kufanya mambo yasipendeza, na yenye chukizo kwa Mungu,” alisema Askofu Mchamungu.
Aidha, aliwataka vijana hao kufahamu kuwa utu wa mtu ni muhimu zaidi katika maisha, na ni vizuri kuthaminiwa kwa sababu ndio zawadi pekee kutoka kwa Mungu.

Rate this item
(0 votes)
Japhet