DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Tanzania inatarajiwa kushinda medali ya dhahabu, katika Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika, kutokana na maandalizi ambayo yamefanyika.
Wanariadha tisa waliokuwa kambi jijini Arusha, kwa dhamira moja ya wazi kwa kuinua bendera ya Taifa juu, wataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo, yanayotarajiwa kufanyika Tallahassee, Florida.