Canberra, Australia
Michuano ya Australian Open itatoa zawadi ya rekodi ya pauni milioni 55, katika mashindano ya mwaka huu, lakini wachezaji wanasemekana wamekata tamaa, kwani haiwakilishi sehemu kubwa zaidi ya mapato yote ya Grand Slam.
Jumla ya pesa za zawadi za A$111.5m, zinawakilisha ongezeko la 16%, ikilinganishwa na mwaka jana, na ndio mfuko mkubwa zaidi wa wachezaji, katika historia ya mashindano hayo.
Mabingwa wa singles watapokea $4.15m (£2.05m), ongezeko la 19% la kiasi ambacho washindi wa 2025, Madison Keys na Jannik Sinner walishinda.
Wachezaji wote wa singles na doubles, wanaoshiriki katika Grand Slam ya ufunguzi wa msimu, watapata ongezeko la chini la 10%.
Mtendaji mkuu wa Tennis Australia, Craig Tiley, alisema kwamba ongezeko hilo linaonesha kujitolea kwao, kusaidia taaluma za tenisi katika kila ngazi.
Hatua hiyo inakuja baada ya kundi la wachezaji, wanaoongoza kuongeza shinikizo, kwenye mashindano ya Grand Slam mnamo Oktoba, kuhusu ongezeko la pesa za zawadi, na ustawi mkubwa wa wachezaji.