Print this page

Santiago Bernabéu de Yeste alivyoacha alama Real Madrid

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Moja ya majina, yanayohusiana kwa karibu zaidi na klabu ya Real Madrid, na maendeleo ya mpira wa miguu barani Ulaya. 
Santiago Bernabéu de Yeste alizaliwa Juni 8, 1895, huko Almansa, Uhispania, na alihusiana na Real Madrid kwa zaidi ya miaka 50, akiwa kama mchezaji, kocha na rais wa klabu hiyo.
Chini ya uongozi wake, Real Madrid ilibadilika kutoka kuwa klabu ya kawaida ya Hispania, hadi kuwa nguvu kubwa ya soka barani Ulaya.
Bernabéu alijiunga na Real Madrid akiwa na miaka 17, mnamo mwaka 1912, na akacheza kama mshambuliaji. 
Alikuwa sehemu ya timu kwa miaka 16, hadi alipoamua kustaafu mnamo 1927, akiwa na umri wa miaka 32. Ingawa hakufanikiwa sana kama mchezaji wa kiwango cha juu, mchango wake halisi kwa klabu ulianza baada ya kustaafu soka.

Rate this item
(0 votes)
Japhet