LONDON, Uingereza
Timu ya soka ya wanawake ya Jersey Bulls, imefanikiwa kuizaba Guildford Saints mabao 30-0, katika mechi ya Ligi ya Soka ya Wanawake ya Kaunti ya Kusini Mashariki mwa Uingereza, maarufu kama Surrey Division One.
Kwa ushindi huo wa maajabu, Bulls imekaribia kufikisha jumla ya mabao 100 ya kufunga, katika mechi zake 11 za Ligi ilizocheza.
Anita Tavares aliongoza kwa mabao tisa, ikiwa ni mara tatu zaidi ya Guildford, ambaye alifunga msimu mzima, huku wachezaji wengine 10 tofauti, wakipata bao katika mchezo huo.