ADDIS ABBA,
Ehiopia
Uaskofu Mkuu wa Ethiopia wa Emdibir, umeandaa kikao maalumu cha mafunzo kinacholenga ulinzi wa watoto, mpango unaotajwa kuwa ni muhimu ikizingatiwa kwamba, zaidi ya theluthi moja ya watoto nchini humo kwa sasa, wanakabiliwa na alama kubwa za udhaifu.
Programu hiyo iliundwa kwa ajili ya walimu wa vyama vya watoto katika Parokia mbalimbali, iliyofunguliwa na Mchungaji Abba Tesfa-Amlak Fikre, Mratibu wa Idara ya Uchungaji.