DAR ES SALAAM
Na Arone Mpanduka
Mchezo wa kikapu wa tatu kwa tatu, maarufu kama 3x3, ni aina ya michezo ya mpira wa kikapu inayochezwa na timu mbili za wachezaji watatu kila moja, kwenye nusu uwanja (half-court) na bango moja la goli.
Mchezo huu una kasi ya juu, unadumu kwa dakika 10, ambapo timu ya kwanza kufikisha pointi 21, inapewa ushindi. Ni mchezo rasmi wa FIBA na sasa ni mchezo wa Olimpiki.