Paris, Ufaransa
Mathieu van der Poel alishinda hatua yake ya tatu ya Tour de France, kwenye mashindano ya mbio za kasi katika hatua ya tisa, ambayo ilifupishwa kutokana na halijoto, kukaribia nyuzi joto 40.
Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 31, alimaliza mbele ya Tobias Johannessen wa Denmark, na Tom Pidcock wa Uingereza, katika kundi la waliojitenga.
Pidcock alikuwa akitafuta ushindi wa pili, katika hatua ya Tour kwenye taaluma yake, lakini alizuiwa na tatizo la kiufundi, mara baada ya mnyororo wa baiskeli yake kuharibika.
Hatua ya tisa ya Jumapili, kutoka Malemort hadi Ussel, ilikuwa karibu kilomita 30 fupi kuliko ilivyopangwa, kwa sababu ya tahadhari nyekundu, kutoka kwa mamlaka ya Ufaransa.
Van der Poel alisema kwamba, ilikuwa siku ngumu sana kwake, kutokana na hali ya joto kuwa kali kuliko ilivyotarajiwa, kutokana na kuzidi tofauti na walivyoanza mashindano hayo mwanzoni.