Print this page

Ifahamu teknolojia ya VS itakayotumika Ligi Kuu msimu ujao

Dar es Salaam

Na Arone Mpanduka

Hivi karibuni Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kupitia kwa Rais wake Wallace Karia, lilitangaza rasmi kuwa kuanzia msimu ujao wa 2026/2027, Ligi Kuu Tanzania Bara itaanza kutumia teknolojia mpya ya VS, ambayo itasaidia kutoa suluhisho la baadhi ya matukio tata ya uwanjani.
Uamuzi huo umekuja baada ya kushindikana kwa teknolojia ya VAR, ambayo ina gharama kubwa za uendeshaji.
VS NI NINI?
Kwa mujibu wa maana ya kawaida katika michezo, VS (Video Support) ni mfumo wa usaidizi wa video, unaotumika kwenye michezo kama vile mpira wa miguu, wavu au tenisi, ambao ni tofauti kidogo na VAR (Video Assistant Referee).
VS (Video Support) ni mfumo wa kidijitali unaoruhusu timu au wachezaji, kuomba marudio ya video kwa maamuzi muhimu ya uwanjani, kama vile goli, adhabu au makosa, sawa na jinsi wanavyofanya katika tenisi (Hawkeye), au mpira wa wavu (Challenge System). 
Tofauti na VAR, ambapo waamuzi wanaweza kuamua kutumia au la, lakini timu zinakuwa na idadi maalumu ya changamoto za kuomba.
INAFANYAJE KAZI UWANJANI?
Wakati mchezo unaendelea, wachezaji au nahodha anaweza kuomba marudio ya tukio tata, na kisha mwamuzi hulazimika kurudia na kufanya maamuzi.

Rate this item
(0 votes)
Japhet