Print this page

Zaka Zakazi awatuliza mashabiki Azam FC

By September 11, 2026 7 0
Thabit Zacharia. Thabit Zacharia.

Dar es Salaam

Na Nicolaus Kilowoko

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya klabu ya soka ya Azam FC, Thabit Zacharia maafuru Zaka Zakazi amegeuka na kumkingia kifua kocha wao, Florent Ibenge kutokana na klabu hiyo kuwa na mwendelezo wa matokeo yasiyofaa uwanjani.
Zaka alisema kwa sasa wanaendelea kufanya maboresho makubwa ya timu yao hivyo mashabiki watulie kwani kocha anaelewa matamanio yao na kuna mabadiliko makubwa ya kiufundi kwa sasa yanafanyika.
Alisema kuwa mara nyingi mashabiki wanatamani kuona klabu yao ikifanya vizuri na hilo wanalifahamu hivyo kupata sare mbili haipaswi wao kukata tamaa na kutoa lawama kubwa kwa uongozi wao.
“Haitoshi kuhukumu katika mechi hizi mbili za mwanzo, mpira unabadilika kwani tumeshuhudia Kombe la Dunia lililoisha juzi tu, Hispania alianza vibaya lakini ndiye aliyekuwa bingwa, hivyo watu wasikate tamaa na kulaumu kwa sare hizi mbili za mwanzo tulizopata,” alisema Zaka.
Alisisitiza kuwa kwa maboresho ambayo kwa sasa wanaendelea nayo mara baada ya kupata mapumziko ya mashindano ya Afrika yamesaidia kocha wao Ibenge kuongeza kitu kwa wachezaji wake ambacho wanaamini kitaisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwa mechi zijazo.
Zaka alisema hata kipindi kile ambacho wanakuwa mabingwa mwaka 2013 mechi zilikuwa kama hivi ambavyo matokeo wanayapata kwa sasa na walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo.
Aliongeza kuwa Ibenge ni kocha mzoefu na mara nyingi mashabiki wanapoona matokeo mabaya hawaangalii wachezaji, kwanza wanaangalia kocha na hiyo ndiyo gharama kwake lakini kwa kikosi walichonacho msimu huu wapo vizuri kutokana na usajili walioufanya.

Rate this item
(0 votes)
Japhet