Barcelona, Hispania
Winga wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Uingereza, Anthony Gordon, ametoa mtazamo wake kuhusu ushindani wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani (Ballon d’Or), akieleza kuwa tuzo hiyo inastahili kutwaliwa na Nahodha wa Uingereza, Harry Kane au winga wa Barcelona, Lamine Yamal.
Gordon alieleza kuwa ingawa si rahisi kwake kutoa hukumu ya moja kwa moja kwani yuko kwenye kiwango tofauti na nyota hao, anaona uwezo wa wachezaji wote wawili ni wa hali ya juu mno.
Gordon alijibu swali lililoulizwa kuwa kati ya Harry Kane ama Lamine Yamal nani anastahili kutwaa Ballon d’Or?
“Mimi si mtu sahihi wa kutoa maoni kuhusu hilo. Ni vigumu kwangu kuzungumzia kwa sababu bado sijafikia kiwango hicho, mimi ni kama nyinyi tu, mimi pia ni shabiki tu ninayefuatilia mchakato huo.”
“Tuzo hii inapaswa kwenda kwa mmojawapo kati yao (Kane ama Yamal). Kwa kijana wa umri wa miaka 19 kufanya kile ambacho Lamine Yamal anakifanya hivi sasa ni kitu cha kushangaza mno. Kane alikuwa na msimu bora wa kihistoria kutokana na idadi kubwa ya mabao aliyofunga pamoja na mchango wake mkubwa kwenye michuano ya kimataifa,” alisema.