Print this page

Nyoso akiri hasira zilimvurugia maisha

Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Juma Nyoso ameweka wazi kuwa yupo tayari kucheza katika timu yoyote ili mradi tu watakubaliana kufanya kazi kwa pamoja.
Nyoso amezungumzia kiwango chake cha soka tangu alipokuwa akicheza kwenye vilabu mbalimbali nchini hadi sasa, akifafanua kuwa hajawahi kutangaza rasmi kustaafu soka.
Alisema kuwa katika kipindi chake alichokuwa anacheza, hasira zilimpelekea pia kushindwa kutimiza baadhi ya mambo yake muhimu na kupelekea hata baadhi ya viongozi wa vilabu kumshangaa kutokana na kuwa alikuwa bora katika eneo la nyuma kucheza lakini alishinda kuzuia hasira.
Nyoso alisema kuwa kuna wakati alipata umaarufu kutokana na matukio aliyokuwa akiyafanya hali ambayo ilikuwa inampa nyakati mbaya sana kwake akiwa uwanjani.
“Kuna wakati hali hiyo ilikuwa inaniumiza sana na kunifanya nishindwe kutimiza mambo mengi na kuna mambo mengine yananitafuna mpaka sasa hasa lile tukio la John Bocco kitu ambacho mpaka sasa kila ukipita unanyooshewa kidole,” alisema Nyoso.

Rate this item
(0 votes)
Japhet